Burudani

Video: Miezi 6 ijayo hakutatokea kelele za msanii kuibiwa kazi – Dkt Mwakyembe

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe Jumatano hii amefunguka kwa kusema kuwa kuna wataalam wa IT ambao wanaandaa mfumo ambao utalinda kazi za wasanii huku akiahidi baada ya miezi 6 hakuna msanii ambaye atasikika akilalamika kuibiwa kazi yake.

Amesema hayo wakati akizungumza na viongozi wa dini nchini katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, ambapo pia alizungumzia mchango wa viongozi hao wadini katika maendeleo ya nchini pamoja na Tanzania ya viwanda.

Dkt. Mwakyembe amesema serikali bado inafanya jitihada mbalimbali katika kuboresha mazingira ya watanzania ambao wanafanya kazi za sanaa pamoja na kunufaika na kazi zao.

“Ndani ya miezi sita ijayo hakutatokea msanii analalamika ameibiwa filamu yake, nimeshasema tunaelekea sehemu nzuri ambayo haya yote yatamalizwa na teknolojia,” alisema Mwakyembe.

Pia waziri aliwapongeza viongozi wa dini kwa kuwaandaa vijana ambayo wamekuwa wakitoa burudani za nyimbo za kuelimisha jamii huku akidai wasanii wa gospel na wale wa kaswida wamekuwa wakitoa nyimbo za kuelimisha jamii na kuhamasisha amani.

“Viongozi wetu tuwe mstari wa mbele katika kurekebisha mavazi ya waumini wetu ili kurudisha maadili ya taifa. Nawaomba msichoke kuimba kuhusu mavazi stahiki yanayoendana na maadili ya taifa. Dk Harrison Mwakyembe.,’ alisema Mwakyembe.

Pia katika mazungumzo yake Dkt. Mwakyembe amewapongeza viongozi hao kwa kutumia ipaswavyo lugha ya Kiswahili katika mafundisho yao kitu ambacho kinachagia ukuaji nzuri wa lugha hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents