Habari

Hizi ndio ajira ambazo zimelengwa kutolewa na Tume ya Ulaya katika bara la Afrika

Hizi ndio ajira ambazo zimelengwa kutolewa na Tume ya Ulaya katika bara la Afrika

Rais wa tume ya Ulaya Jean-Claude Juncker amependekeza kuwepo kwa muungano mpya na Afrika, kuboresha uhusiano wa kiuchumi na pia kuongeza uwekezaji na ajira.

European Commission President Jean-Claude Juncker speaks during a media conference at EU headquarters in Brussels on Monday, June 29, 2015. European Commission President Jean-Claude Juncker says he felt a betrayed by Greek Prime Minister’s Alexis Tsipras surprise call for referendum last weekend. (AP Photo/Virginia Mayo)

Kwenye hotuba yake ya kila mwaka Bw Juncker alisema mpango huo utasaidia kubuniwa mamilioni ya ajira barani Afrika katika kipindi cha miaka mitano inayokuja.

Maoni ya Bw Juncker yanahusu kile anachokiita biashara huru kati ya mabara. “Suala hapa ni kuboresha mikatati iliyopo sasa ambayo inazipa karibu nchi zore za Afrika uwezo wa kufikia masoko ya Ulaya bila kodi.”Pendekezo hilo pia linawapa fursa zaidi watu kutoka afrika kuongeza maarifa kwa mfano kwa kusomea viuo vikuu vya Ulaya.

EU inapendekeza Jumla ya euro bilioni 40 katika kipindi cha miaka saba hadi mwaka 2021. “EU inataka kupanua uhusiano wake na Afrika ambayo ni sehemu muhimu sana duniani.”

Pia Juncker alitangaza mipango ya EU kutuma walinzi wa mipaka 10,000 kukabiliana na uhamiaji haramu ifikapo mwaka 2020. Bw Jucker alisema EU inahitaji kuwa salama kutoka kwa vitisho vingi vinavyoikumbwa.

European Commission’s President Jean-Claude Juncker delivers a speech as he makes his State of the Union address to the European Parliament in Strasbourg, eastern France, on September 14, 2016. / AFP / FREDERICK FLORIN (Photo credit should read FREDERICK FLORIN/AFP/Getty Images)

“Ni Ulaya dhabiti tu na yenye nguvu inayoweza kuwalinda watu wake kutokana vitisho vya nje na vya ndani – kutokana wa ugaidi na mabadiliko ya hali ya hewa.”

Mashirika ya Frontex na lile na ulinzi wa mipaka na pwani la Ulaya kwa sasa yamewajiri walinzi 1,600 kutoka Ulaya, kwa hivyo idadi mpya inayotajwa na Juncker ni ongezeko kubwa.

European Union Commission President Jean-Claude Juncker delivers a press conference following a Special Meeting of the European Council at the EU Council building in Brussels on April 29, 2017.
The EU needs a “serious British response” to its demands to protect citizens’ rights, EU President Donald Tusk said on April 29, setting terms for launching new ties with the bloc after Brexit. / AFP PHOTO / THIERRY CHARLIER (Photo credit should read THIERRY CHARLIER/AFP/Getty Images)

Bw Juncker zaidi alipendekeza kubuniwa shirika linahusika na kutoa hifadhi barani Ulaya amabalo litatoa msaada kwa nchi zinazowapa hifadhi watafuata hifadhi.

Alisisitiza hitaji la kuwepo njia halali za kuingia Ulaya. “tunahitaji wahamiaji wenye ujuzi,” alisema.Kutakuwana sheria mpya za kutoa makala zinazohusuhu ugaidi kutoka kwa mitandao ndani ya saa moja.Mitandao itahitajika kuwa na njia za kufuta kile kilicho kwenye mitandao laikini haijulikani ni mbinu gani zitatumiwa.

KELEBIJA, SERBIA – 2017/03/23: A Syrian family walks towards the gate to cross to Hungary as they applied for asylum at the Kelebija border crossing point. Hungary passed a Stop Soros law that makes it illegal to help undocumented migrants. (Photo by Omar Marques/SOPA Images/LightRocket via Getty Images)

Pendekezo lililoandikwa linaamaanisha kuwa makampuni ambayo yashindwa kutimiza matakwa hayo yatakabiliwa na faini ya hadi asilimia 4 ya pato lao la mwaka mzima.

Uchumi wa ulaya umekuwa kwa mwaka mitano mfululizo, “hakujakuwa na idadi kubwa ya wanawake na wanaume milioni 239 kuwa kwenye ajira barani Ulaya,” Bw Juncker alisema.”Ukosefu wa ajira kwa vijana ni asilimia 14.8. Ni hali ya juu zaidi lakini pia ya chini zaidi tangu mwaka 2000.”

Chanzo BBC

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents