Habari

Hofu yatanda, Mamia ya watu hawajulikani walipo, baada ya maporomoko ya ardhi Uganda

Maporomoko ya ardhi Uganda: Kuna hofu huenda idadi ya waliyofariki ikaongezeka

Zaidi watu 50 wamepoteza maisha kutokana na maporoko ya ardhi na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha mashariki mwa Uganda. Mamia ya watu bado hawajulikani walipo huku maafisa katika wilaya ya Bududa wakihofu kuwa idadi ya waliopoteza maisha huenda ikaongezeka.

Walioshuhudia mkasa huo wanasema kuwa mwamba ulidondoka mtoni na kupasua kingo za mto hali iliyosababisha maji yaliyochanganyikana na matope kuanza kusomba watu vijijini.

Serikali imesema vikosi vya uokoaji vimepelekwa katika eneo hilo karibu na mpaka wa Uganda na Kenya lakini miundo mbinu ya barabara na daraja iliyoharibiwa imelemaza shughuli za uokozi.

Picha kutoka eneo la tukio zinaonyesha watu wakitoa miili kutoka ndani ya tope na kuweka kando Maporomoko mengine ya odongo yalishuhudiwa katika eneo hilo la Bududa yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 300 mwaka 2010. Mwanahabari wa kujitegemea Shwahib Ibrahim, ameiambia BBC kuwa baadhi ya wakaazi mpaka sasa hawajui wapendwa wao wako wapi.

Ibrahim pia amesema shirika la msalaba mwekundu limekuwa likiwasaidia waathiriwa wa mkasa huo tangu jana.

Kwa upande wake msemaji wa shirika la Msalaba mwekundu Irene Nakasiita amesema “Maji yalipoanza kuteremka chini ilibeba mawe makubwa ambayo iliharibu nyumba za watu,” Kufuatia mikasa iliyopita, watu waliiamriwa kuhama eneo hilo lakini wengi wao walirejea kwa kuvutiwa na ardhi yenye rutuba na upendo wa makaazi yao ya asili.

Chanzo BBC

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents