Burudani

Huenda Fid Q akatoa Fresh Remix nyingine

Msanii wa hip hop Bongo Flava, Fid Q amesema huenda ikatoa remix nyingine ya ngoma ‘Fresh’.

Fid Q ambaye hapo jana alitoa remix ya ngoma hiyo kwa kuwashirikisha Diamond Platnumz na Rayvanny, ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa sababu kuwaza mpango huo ni kutokana kuna baadhi ya wasanii walihitaji kuwepo katika remix.

“Nilipotoa Fresh ZaiiD aliniambia please kama utatoa remix na mimi niwepo, kwa hiyo ilipokuja kutokea hii nyingine siyo kama nimemsahau, hapana kuna mipango mingine inafanyika, huenda kukawa na remix nyingine lakini alinishtua kwamba nataka kuwepo na ni moja ya marapa ambao napenda sana michano yao na bila shaka hato-disappoint,” amesema.

Ngoma ya Fresh original ilitoka August 13 ambayo ilikuwa ni siku ya kumbukumbu yake ya kuzaliwa, video ya ngoma hiyo hadi sasa ina views 171,853 katika mtandao wa YouTube.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents