Burudani

Idris Sultan: Nilikuwa nawapenda Wema na Samantha kwa wakati mmoja, ‘I was a very bad guy

Idris Sultan alikuwa kwenye ‘love triangle’ na alishindwa kujinasua kwa muda mrefu sababu alikuwa akiwapenda wasichana wawili – Wema Sepetu na Samantha wa Afrika Kusini.

12558814_1687140004860922_1425406858_n

Staa huyo alifunguka kirefu usiku wa kuamkia leo kwenye kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM. Idris alisema kutokana na kushindwa kuushawishi moyo wake uchague moja, anakiri kuwa hakuwa mtu mzuri na alimliza zaidi Wema.

“She [Wema] a woman ambaye I love so much halafu kila siku nilikuwa namfanya analia, sio kwamba ilikuwa inanifanya niweze kulala vizuri au nini, no. Halafu huku kwingine there is another woman [Samantha] ambaye I am so in love with.”

Idris anasema baada ya kuona kuwa yupo na Wema lakini bado anaendeleza uhusiano wake na Samantha ilimbidi amuombe wausimamishe kwanza kuepuka kumchukulia kama mchepuko wakati alikuwa akimpenda.

Anasema hapo ndipo uhusiano wake na Samantha ukawa wazi na kila mtu akawa anaujua. Hata hivyo alisema pamoja na hivyo walipokuwa wakikutana waligundua kuwa bado walikuwa wakipendana na kila mtu wao wa karibu aligundua.

Idris anasema anaamini Wema alianzisha uhusiano na Luis Munana kama njia ya kumuumiza. Mara nyingi walipokuwa wakienda kwenye ‘double date’ Wema alikuwa akimuumiza Idris makusudi kwa kumbusu Luis hadharani.

“Wakifika kwenye dinner yaani yeye na Luis yaani hata chakula hakiliki wamebaki wanakiss, too much yaani,” alisema Idris. “Yaani walikuwa wanafanya telemundo kwasababu ilikuwa too much on my face.”

Idris anasema alikuja kuachana na Samantha baada ya mara nyingi kujikuta wakigombana sana kutokana na kila mmoja kuwa na mambo yanayomkera mwenzake. Aligundua kuwa walikuwa na furaha zaidi wakiwa marafiki na sio kama wapenzi.

Anasema siku wameachana na Samantha rasmi ndio ilikuwa siku ya siku ya kuzaliwa ya Wema na alienda kwenye sherehe yake iliyofanyika kwake Kijitonyama na aliamua kumweleza ukweli wa moyo wake lakini anasema alishangaa kumuona jinsi ambavyo alikuwa akifurahia. Hicho ni kipindi ambacho Wema alikuwa na Luis na aliumia sana.

Kupunguza story ndefu kuwa fupi, wawili hao waligundua kuwa wanapendana na waliamua kuanzisha safari rasmi ya uhusiano na sasa wanatarajia kupata mtoto.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents