HabariUncategorized

Ifike mahali turuhusu mtu akihama chama ahame na ubunge wake – Nape Nnauye

Mbunge wa jimbo la Mtama tiketi ya CCM, Nape Nnauye amefunguka kuzungumzia hama hama ya wabunge na madiwani wengi kutoka nyama vya upinzani kwenda chama tawala cha CCM.


Malalamiko ya wengi katika mitandao ya kijamii yanadai kwamba hama hama hiyo imeweza kuisababishia serikali gharama kubwa za kurudia uchaguzi.

Akiongea na Azam TV Ijumaa hii, Mhe Nape amedai ingawa ni jambo gumu lakini angependa wabunge ambao wanahama vyama waruhusiwe kuendelea na nafasi zao kwa kuwa wamechaguliwa na wananchi.

“Hii kitu nadhani ina ukakasi, najua haivunji sheria lakini ina ukakasi na kama ina ukakasi nadhani umefika wakati pengine tukatengeneza forum ya kupitia sheria zinazoongoza huu mchezo kwenye mfumo wa vyama vingi,”

“Kwa mfano ifike mahali turuhusu mtu akihama, ahame na ubunge wake”

Wiki iliyopita tulishuhudia mbunge wa Ukonga Mwita Waitara akihama CUF na kuhamia CCM na wiki hii kamati kuu ya chama hicho imempitisha kugombea ubunge.

Related Articles

31 Comments

  1. Unajua kipindi unapigiwa kura,kuna wapiga kura wa aina kama tatu hivi mosi..kuna wapiga kura wa mapenzi ya yachama,yaan anakupigia kura kwa sababu anakipenda chama pil kuna mpiga. Kura kwa mapenzi ya mtu husika (mgombea)na 3..kuna wapiga kura wa mizuka yaan yeye anafuata mkumbo…sasa je wale wa mapenzi ya chama utakuwa umewatendea haki

  2. Kamaanisha wanatia hasara kodi za wananchi bora kama vipi wakihama chama weather wagharamie uchaguzi kwa Pesa zao za mifukoni au ikishindikana basi waruhusiwe kuhama na ubunge wao ili kuepuka kuwaumiza wananchi wabaolipa kodi zao kwa maendeleo ya kijamii na nchi kwa ujumla na sivyo unavyofikiria wewe

  3. Hapana….hapana,binafsi hilo halitasaidia,napendekeza iwe hivi,kama mtu akihama chama basi yule aliyemfuata yaan wa pili wakati wa uchaguzi ndo awe mbunge bila kujari chama.
    La sivyo watu watahama mala 20.

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents