Aisee DSTV!
SwahiliFix

Jaguar aibua jipya lingine nchini Kenya, Vijana wampongeza wazee roho juu

Mbunge wa Jimbo la Starehe nchini Kenya, Jaguar ameibua mijadala nchini humo baada ya kuwasilisha hoja  kuwa umri wa kustaafu upunguzwe.

Jaguar

Jaguar amependekeza umri wa kustaafu upungue kutoka miaka 60 hadi 50 ili kuongeza ajira kwa vijana.

Akitoa mapendekezo hayo leo Septemba 12, 2019, Jaguar amesema kuwa Kenya inakabiliwa na uhaba wa ajira kwa asilimia 55, Na wahanga wakubwa ni vijana.

Kwa mujibu wa takwimu alizozitoa, Amesema vijana 800,000 wanaingia kwenye soko la ajira nchini Kenya lakini wanaopata nafasi ni vijana 70,000.

Endapo mabadiliko hayo yatafanikiwa, Nafasi 25,000 zinazotumikiwa na watumishi wa umma wenye umri kati ya 50-60, zitakuwa wazi.

Tamko hilo, Limeungwa mkono na vijana wengi kwenye mitandao ya kijamii nchini Kenya wakidai kuwa litapunguza tatizo la ajira.

Hata hivyo, Tamko hilo huenda lisipite kwa urahisi kwani watu wenye umri mkubwa nchini humo, Wamekuwa wakileta pingamizi.

 

Miezi miwili iliyopita, Jaguar alishambuliwa mtandaoni kwa kutoa kauli ya kibaguzi, Jambo ambalo lilimfanya awaombe radhi wafanyabiashara wa kigeni nchini humo.

Soma zaidi – http://bongo5.com/mbunge-jaguar-akamatwa-na-polisi-kenya-kwa-uchochezi-na-ubaguzi-video-06-2019/

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW