Habari

Jaji Warioba awachana viongozi nchini

Waziri mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba, ametoa wito kwa viongozi waliopewa dhamana ya uongozi katika ngazi mbalimbali nchini kutatua matatizo ya wananchi na sio kujinufaisha wenyewe.

warioba-e1398330806759

Ametoa wito huo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza katika muadhara wa tatu wa uzinduzi wa hifadhi ya nyaraka za kumbukumbu mbalimbali za hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere maarufu kama ‘Kavazi la Mwalimu Nyerere’

“Ukiona viongozi wetu, na huku nyuma viongozi hawa wakina mzee Kahama, kazi yao ilikuwa ni kuhangaika na matatizo ya nchi, kazi yao ilikuwa ni kuhangaika na matatizo ya taifa, kazi yao ilikuwa ni kuhangaika na matatizo ya wananchi,” alisema.

“Siku hizi viongozi wanachukua matatizo yao wanataka wananchi wayashughulikie, yaani viongozi wanakwenda kushtakiana kwa wananchi, wamechaguliwa washughulikie matatizo ya wananchi, badala yake wanagombana wanaenda kushtakiana kwa wananchi, kwanini walichaguliwa? Mi nadhani mfanye kazi,” alisisitiza Mzee Warioba.

Kavazi la Mwalimu Nyerere ni kituo huru kilichoanzishwa ndani ya tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTEC)mwaka 2014 kwa lengo la kuhifadhi nyaraka mbalimbali za hayati baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents