Habari

Japan ipo tayari kukarabati shule zilizobomoka kufuatia tetemeko la ardhi

Waziri mkuu, Kassimu Majaliwa, amekutana na kufanya mazungumzo na balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshinda,ambaye ameeleza kuwa serikali ya Japan ipo tayari kukarabati shule zilizoathiriwa na tetemeko la ardhi.

1-1

Balozi Yoshinda ameyasema hayo Jumatatu hii alipokutana na waziri mkuu ofisini kwake jijini Dar es Salaam,kwaajili ya kuzungumzia maafa yaliyotokea mkoani Kagera.

Waziri mkuu ameishukuru serikali ya Japan kwa hatua hiyo na kukiagiza kitengo cha maafa kilichopo chini ya ofisi yake kuwasiliana na ubalozi wa Japan nchini,na kuwasilisha orodha ya shule zilizoharibika pamoja na mahitaji ya dharura.

Pia alipokea msaada wa tani 2.5 za mchele,magodoro 200,mabranketi 100,na fedha taslimu shilingi millioni kumi ili kusaidia wananchi walioathirika wa tetemeko la ardhi.

Msaada huo umetolewa na wadau mbalimbali akiwemo afisa utumishi wa kampuni ya Chang Qing internation investment, Anna Jiang aliyetoa magodoro 200 yenye thamani ya shilingi millioni sita, na mkuu wa fedha wa kitengo cha Exim bank, George Shungusho, aliyetoa shilingi millioni 10, katibu mkuu wa chama cha urafiki kati ya Tanzania na China, Joseph Kahama aliyetoa mchele tani 2.5 na mablanketi 100.

Waziri Majaliwa ameendelea kuwataka wananchi wengine kuendelea kujitokeza kutoa misaada kwa waathirika hao na alisema kuwa ni janga ambalo halijawahi kutokea nchini Tanzania.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents