Burudani

Jay Moe kuipeleka ‘Stori Tatu’ kwenye filamu

Msanii wa muziki wa hip hop, Jay Moe ameweka wazi mpango wake wa kuandaa filamu kupitia stori ya wimbo wake wa zamani ‘Stori Tatu’ alioutoa miaka 10 iliyopita.

Rapa huyo ambaye aliwahi kushiriki na kufanya vizuri kwenye filamu ya Girlfriend akiwa na King Crazy GK pamoja na TID Mnyama, amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwaajili ya project hiyo ambayo amedai itakuwa na mambo makubwa.

“Nimefikiria kurudi kwenye filamu lakini kwa kutumia wimbo wangu ‘Stori Tatu’ kwa sababu kila stori moja inajitegemea na ina stori yake. Kwa hiyo hata ikitokea nafasi tunaandika movie ikaitwa ‘Stori Tatu’ itafanya vizuri kwa sababu sasa hivi unaona kuna matukio mengi ambayo yanatokea ndani ya mkoa wa Dar es salaam lakini sisi tuliyasema miaka kadhaa iliyopita kupitia wimbo huo,” Jay Moe alikiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM.

Aliongeza, “Kwa hiyo najua hiyo movie itakuwa na mafundisho kwa sababu ndani yake nilizungumzia vitu vingi, watu wengi wataipenda, ina sehemu nyingine inaelezea mshkaji wangu Inno ambaye ni mwathirika wa dawa za kulevya, kwahiyo wimbo ulitoka mwaka 2007 ni miaka 10 mpaka sasa lakini ujumbe wake unafaa leo kuonekana kwenye picha,”

Moe ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Nisaidie Kushare’ hakuweka wazi ni lini filamu hiyo itaanza kuandaliwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents