Burudani

Jay Z kumsainisha Ice Prince Roc Nation? Interview hii na Power 105.1 inalo jibu (Video)

Kwa msanii wa Afrika akienda nchini Marekani na kufanyiwa interview na kipindi cha The Breakfast Club cha Power 105.1 (redio inayosikilizwa zaidi jijini New York sambana na Hot 97), si kitu cha rahisi.

https://www.youtube.com/watch?v=7VcNsw2d6Rg

Ice Prince anaweza kuwa ndio msanii wa kwanza wa Afrika kufanyiwa mahojiano kwenye kipindi hicho maarufu. Kwenye mahojiano hayo Ice Prince ameelezea uhusiano wake na label ya Jay Z, Roc Nation.

“Nina uhusiano mzuri sana na Rock Nation,” alisema Ice Prince.

“Tupo kwenye mazungumzo, tupo kwenye mazungumzo serious muda huu,” aliongeza.

Ice-Prince-Jay-Z-600x600

Akizungumzia picha aliyoweka Instagram akiwa na Jay Z, Ice Prince alisema kukutana na rapper huyo kilikuwa ni kitu muhimu maishani mwake.

Wawili hao walikutana jijini New York kwenye ofisi za Roc Nation.

“Jay Z aliniambia kuwa mimi ni mtu mkubwa,” alisema Ice.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents