Moto Hauzimwi

Jhene Aiko afunguka kuhusu mahusiano yake na Big Sean (+Video)

Msanii Jhené Aiko amefunguka kuhusu mahusiano yake na Big Sean. Akizungumza na BBC Radio 1Xtra, Jhene alisema kuwa uhusiano wao umepitia vikwazo kadhaa.

“Tulikuwa marafiki mwaka ambao nilifiwa na kaka yangu na ndipo tulipo anza kufanya kazi kwa pamoja ikiwemo ‘Beware’ na ‘I’m Gonna Be.’ Alitaka kunipeleka on a date. Nilikuwa nina mchumba, lakini bado nilikwenda … kama rafiki.” Alisema Jhene Aiko.

Mwimbaji huyo amejichora tattoo ya uso wa Sean katika mkono wake

Uhusiano wake na ex ulimalizika mara tu baada ya kujua kwamba mwanaumee wake alioa kisiri, lakini ilikuwa ni vigumu sana kwa yeye kutoka na Big Sean, ambaye alikuwa tayari katika mahusiano na mtu mwingine. “alikuwa na girlfriend niakonani sawa tu bado sisi ni marafiki na tulikuwa tukifanya show kwa pamoja na pia kurekodi nyimbo.” aliongezea Jhene.

Wakati huo huo wa mahojiano, Jhené aliulizwa kama Sean eats the booty like groceries. Lakini Aiko alisema kuwa hapendelei kabisa swala hilo. “Kwa sababu tu nimekiimba hicho kitu sio kama nakipenda na ilikuwa kama utani kwangu na niliimba hivyo ili kuunogesha muziki wa ‘Post to be’

Na Raheem Rajuu

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW