Burudani ya Michezo Live

Jose Chameleone: Kiswahili nilichojifunza miaka 10 iliyopita kimenifikisha hapa

jose mayanja

Unaweza kuwa ni miongoni mwa watu wanaokichukulia poa Kiswahili na kudhani kuwa kujua Kiingereza ndio dili! Muulize Jose Chameleone jinsi Kiswahili kilivyobadilisha maisha yake. Kupitia Twitter, Jose Chameleone amekiri kuwa Kiswahili alichojifunza akiwa nchini Kenya miaka 10 iliyopita kimemfikisha hapo alipo leo akiwa mwanamuziki tajiri na mwenye mafanikio makubwa barani Afrika.

“The SWAHILI I learnt 10yrs ago brought mi here. Am JOSEPH,” ametweet.

Chameleone anajulikana kwa hits nyingi alizoimba kwa Kiswahili na kama ukikutana naye na akakuongelesha Kiswahili huwezi kudhani ni Mganda, anakijua vilivyo.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW