Burudani

Joti afunguka na kutaja muda wa kurejea tena Comedy Show baada ya kupotea kwa muda (+Video)

The Comedy Show kurejea tena machoni mwa washabiki

Mchekeshaji maarufu nchini bwana Lucas Mhuvile alimaarufu Joti amefunguka na kuelezea sababu ya kipindi cha vichekesho ambacho walikuwa wanakifanya kila siku ya jumapili wakiungana wasanii sita kukaa kimya. Mchekeshaji huyo amefunguka wakati anapiga stori na Bongo five siku ya uzinduzi wa vichekesho ambavyo vimerejea kwa sasa ikiwa ni msimu wa pili vinavyojulikana kwa jina la Mwantumu.

Joti amefnguka baada ya kuulizwa kwamba kwanini vichekesho hivyo ambavyo walikuwa wakivifanya kila siku ya jumapili wakiungana wasanii sita ambao ni Joti,Msanaja,Mpoki,Vengu,Wakuvanga na Makregani,ambao kwa sasa kila mmoja anafanya kazi yeye kama yeye.

Joti amefunguka na kusema “Comedy Show itarejea muda sio mrefu watu watarajie kuwaona Masanja,Joti,Mpoki Wakuvanga,Makregani na Vengu wakifanya kazi pamoja tena”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents