Habari

Judy Boucher kutumbuiza leo jijini Kampala


Wapenzi wa muziki wa Uganda leo wana bahati ya kumshuhudia mwanamuziki mkongwe wa nyimbo za taratibu kutoka Marekani, Judy Boucher.
Mwanamuziki huyo aliwasili mjini Kampala jumanne wiki hii na leo atashiriki kwenye tamasha la hisani litakalofanyika Serena Hotel.
Boucher alisema atatumbuiza nyimbo zilizompa umaarufu za ‘Cant Be with You Tonight’ na ‘Mr. Dram Maker’.
Akiongea na mtandao mmoja nchini Uganda, Boucher amesema kila aimbapo nyimbo hizo, umati wa watu hugeuka kama wehu kwakuwa huzipenda sana.
Baadhi ya fedha zitakazopatikana kwenye tamasha hilo zitatumika kujenga makazi maalumu ambayo yatahudumia wazee.
Nyimbo zingine maarufu za mwanamuziki huyo ni pamoja na Tears on My Pillow, Dreaming of a Little Island, Stand by Your Man na If My Heart Had Windows.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents