Burudani

Juma Nature kuadhimisha miaka 16 kwenye muziki kwa kuja na ‘Komaa Concert’ May 30

Tamasha kubwa la kuadhimisha miaka 16 ya JUMA NATURE pamoja na hitimisho la sherehe za mwaka mmoja za 93.7 EFM linalofahamika kama KOMAA CONCERT litafanyika rasmi Jumamosi hii, May 30, kwenye viwanja vya Dar Alive –Mbagala.

DU7C5576
Juma Nature akiongea na waandishi wa habari

Tamasha hilo limeandaliwa na Juma Nature akishirikiana na EFM kwa lengo la kuwaburudisha mashabiki wake na wasikilizaji wa kituo hicho ikiwa ni sehemu ya kuwashukuru mashabiki kwa ushirikiano wao kwa kipindi chote hicho.

Mashabiki watapata burudani kutoka kwa Nature ambaye atatumia dakika 180 akiwa jukwaani kuhakikisha anakonga nyoyo za mashabiki wake kwa kuimba nyimbo zake zote kali zilizofanya vizuri na kusindikizwa na wasanii kibao.

DU7C5566

Wasanii watakaomsindikiza ni pamoja na Profesa Jay, Shetta, Snura, Makomando, Msagasumu na wengine wengi.

“Tunaamini Juma nature ni msanii mwenye kipaji kikubwa na aliyewahamasisha wasanii kibao kuingia katika muziki huu wa kizazi kipya hivyo anastahili kupewa heshima kubwa kwa mchango wake mkubwa katika kukuza muziki wa kizazi kipya,” imesema taarifa ya EFM.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents