Burudani

Kadigo na Young Killa kukamilisha Rap City Mwanza ya Fid Q?

Kadigo akiwa na Fid Q

Kwa muda mrefu Mwanza haijapata mkali mpya wa michano aliyepewa salute na Tanzania nzima kwa uwezo wake kama ilivyo kwa Fareed Kubanda.

Pengine matumaini ya Mwanza kupata ‘icon’ mwingine wa Hip Hop yameanza kuonekana.

Kutana na rappers wawili wa Mwanza ambao Fid Q amewakubali na kuamua kuwasaidia Tanzania iwajue, Kadigo na Young Killa.

Young Killa alipotumbuiza kwenye show ya Fiesta Dodoma

“Kadigo ni msanii mwenye potential kubwa sababu ana style nyingi na anafanya tofauti na wanavyofanya wasanii wengi, inshort ukimchukua Kadigo ukamweka na Young Killa unakuwa unapata ule ukamilifu wa rapcity Mwanza, unajua haiwezi kuwa rap city kama anayewakilisha anakuwa ni Fid Q tu ,” Fid ameiambia Bongo5 leo.

“Ujio wa Kadigo na ujio wa Young Killa ni vitu ambavyo vinanifanya mimi nipate faraja sana nione kwamba ile dream ya kuanzisha Mwanza Rap City inaanza kuwa kweli kwasababu watu wanakuja na style zao unique , uandishi wao ni wa tofauti.”

Fid aliongeza, “kuna project fulani ambazo zipo chinichini ambazo ni mapema sana kuongea chochote lakini cha msingi ambacho nataka muelewe ni kwamba nafurahi kwamba menejimenti ina wakali wangu kama Kadigo na Young Killa.”

Young Killa alichaguliwa kwenye shindano la Super Nyota la Fiesta ya mwaka huu kutoka Mwanza na amekuwa akizunguka nchi nzima na Super Nyota wengine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents