Burudani

Kala Jeremah, Afande Sele na Steve Nyerere waizungumzia Nyerere Day

Ni miaka 14 leo tangu kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Julius Kambarage Nyerere. Kala Jeremah, Afande Sele na Steve Nyerere wameungana na Watanzania wengine kumuenzi na kutoa maoni yao kuhusu udhaifu wa serikali ya awamu ya nne ukilinganisha na utawala wa Rais huyo wa kwanza wa Tanzania.

Mwalimukambarage

Hivi ndivyo walivyozungumza.

Kala Jeremiah

Kuna mambo mengi yanatokea hasa ufisadi wa macho kwa macho yani ufisadi ambao unaonekana ambao wakati wa Nyerere usingetokea kwasababu aliwajengea wizi ni kitu kibaya na ile misemo yake aliyekuwa anasema ukisha tenda kitu fulani huwezi kukiacha ni kama kula nyama ya mtu utaendelea. Nadhani kulikuwa kuna woga ambao ulikuwepo ambao sasa hivi haupo kabisa. Sasa hivi kuna ule ufisadi wa macho kwa macho ambao tunajua kabisa watu wameiba kiasi gani lakini bado tunawaacha ndio maana kwenye wimbo wa Taifa nilioimba mimi na dada yangu Nakaaya tuliimba Nyerere angekuwepo angesemaje ,angeonaje, je wangemwambiaje? Kwahiyo naamini Baba wa Taifa J.K.Nyerere tutamkumbuka daima.

Steve Nyerere:

Nataka kuwaambia Wananchi,Nyerere alisisitiza amani ya Tanzania, Nyerere alisema tukigawanyika hatutaweza kuijenga Tanzania yetu. Tuchaguwe viongozi ambao wanaweza wakatufaa kwa maendeleo yetu. Nakumbuka Nyerere alisisitiza kilimo,alisema rushwa ni aduI wa haki, kwaiyo mimi naona tukitumia falsafa za Nyerere tutafika mbali sana.

Afande Sele:

Nyerere katuachia hotuba zake ambazo tukizitumia nchi yetu itaendelea, lakini Watanzania hatuyafuati aliyoyaongea Nyerere. Watanzania wavivu kusoma vitabu, wakati Nyerere katuachia vitabu vingi ambavyo tukivisoma vitabadili maisha ya Watanzania. Kwa upande wa serikali kiukweli wanatuangusha, viongozi wetu hawana uzalendo kila mmoja anataka kufanya mambo kwa maslahi binafsi kwa hali hii hatuwezi endelea kabisa.


Hizi ni baadhi ya kauli alizowaHi kusema hayati J.K.Nyerere wakati wa uhai wake.

Amini nawaambieni enyi Waswahili wachache mnaotawala; mnategemea kweli kuwa mtawaongoza Watanzania kwa lazima wakati wamepoteza matumaini, na mtegemee kuwa watasalia wamekaa kimya kwa amani na utulivu?

Wakati wengi wa wananchi wanapopoteza matumaini unajenga volcano. Volcano hii italipuka siku moja. Labda kama watu hawa ni wajinga.

Hivyo basi Watanzania watakuwa ni wajinga na mataahira, kama watakubali kuendelea kukandamizwa na watu wachache (viongozi) katika nchi yao wenyewe

Siku inakuja ambapo watu watachagua kifo kuliko fedheha na ole wao wale watakoiona siku hiyo! Na ole wao wale watakaoifanya siku hiyo isiepukike. Natumaini na kusali kuwa siku hiyo kamwe haitofika

Leo Oktoba 14 2013, Taifa linaomboleza mwaka wa 14 tokea Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliyefariki dunia katika hospitali ya Mtakatifu Thomas mjini London, Uingereza.

Happy Nyerere Day.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents