Burudani

Kala Jeremiah: Dkt. Mwakyembe afute kauli yake

Msanii wa Hip Hop, Kala Jeremiah amemuomba Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe kuifuta kauli yake kuwa wasanii waache kuimba nyimbo za siasa kwani inaleta tabaka katika jamii.

Kala Jeremiah

Akizungumza na kipindi cha Planet Bongo amesema aliona kauli hiyo haipo sawa kwani inatengeneza gapa kati ya wanasiasa, wanamuziki na jamii, na kuongeza wanamuziki na siasa ni kitu kimoja kinachounganisha jamii na muda mara zote wanakutana kwenye jamii.

“Bila jamii nisingehusika na masuala ya siasa lakini ninapotaka kuimba wimbo wowote wa kuisaidia jamii yangu kama wajane, watoto yatima lazima niingie huko. Unaweza kuona wimbo wangu wa mwisho wa ‘Wana Ndoto’ ni wimbo wa kutetea watoto yatima lakini ndani niliingiza kuwa wana ndoto ya kugombea Urais kama Rungwe, wana ndoto za kuwa meya, wabunge, waziri tayari nimeingia kwenye siasa.

“Kwa hiyo anapotuzuia kuingia kwenye siasa ni kwamba anatuzuia kufanya muziki wa kijamii na moja kwa moja anakuwa anatulazimasha tuimbe mapenzi, serikali na jamii itapa hasara kubwa. kwa mfano wimbo wangu Wana Ndoto,  nilivyoutoa nimepata comment nyingi kutoka kwenye mashirika ambayo yanahusika na watoto wanasema ujumbe nilioufikisha ingekuwa wao wangetumia billion of money kufikisha ule ujumbe lakini mimi nimefanya bure,” amesema Kala Jeremiah.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents