Habari

Kama James Bond akiwa mweusi ni muigizaji gani angefaa?


Tangu filamu ya kwanza ya James Bond ya Dr. No iliyofanywa na Sean Connery mwaka 1962 mpaka Skyfall ya Daniel Craig mwaka huu waigizaji wote wamekuwa wazungu ambao wengine ni pamoja na George Lazenby, Roger Moore, Timothy Dalton na Pierce Brosnan.

Hakuna muigizaji wa kiafrika ambaye amepata nafasi ya kuigiza uhusika huo. Bad news ni kuwa hakuna uwezekano wa hivi karibuni Daniel Craig kumpa kijiti muigizaji mwingine kwakuwa baada ya Skyfall tayari amesaini mkataba wa kuigiza filamu zingine mbili za Bond.

Lakini je kama muigizaji mwenye asili ya kiafrika akipewa shavu hilo ni nani angefaa? Haya ni baadhi ya majina ambayo tunahisi yanaweza kufit uhusika huo.

1. Denzel Washington – kwenye picha hapo juu

2. Idris Elba

3.Omari Hardwick

4. Will Smith

5.Derek Luke

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents