Burudani

Kama wewe ni rapper mkali unastahili chorus kali – Stereo

Rapper Stereo amedai sababau ya yeye kukaa kimya kirefu bila kusikika kimuziki ni kutafuta namna ya kufanya muziki wake kibiashara zaidi.

Stereo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Mpe Habari’ aliomshirikisha Rich Mavoko amekiambia kipindi cha Papaso cha TBC FM kuwa kwa sasa anahitaji kufanya muziki mzuri.

“Nahitaji kufanya muziki katika namna ya kibiashara zaidi, kufanya ngoma kali, video kali, iende kwa watu ifike mbali mwisho wa siku kieleweke. Halafu kama wewe ni rapper mkali unastahili chorus kali,” Stereo amesema.

Ameongeza, “Sijawahi kulipa msanii katika kolabo, kinachotokea ni kwamba mara nyingi wasanii ambao ninahitaji kuwashirikisha huwa wanapenda kazi zangu, kwa hiyo huwa hata sio ngumu”.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents