AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Kanye adai kofia yake ‘Make America Great Again’ inampa nguvu maradufu

Mwanamuziki maarufu duniani, raia wa Marekani kanye west ameisifu kofia ya rais wa nchi hiyo Donald Trump, baada ya kuivaa na kujihisi mwenye nguvu na bora zaidi.

Kofia hiyo iliyoandikwa “ifanye Marekani kuwa kubwa tena” aliivaa alipo kutana na rais Trump Ikulu ya Marekani kwa chakula cha mchana na kujadili juu ya kuboresha mambo mbalimbali ikiwemu suala la wafungwa, ubaguzi wa rangi pamoja na haki za wasanii nchini humo.

Kanye west alizungumza kwa dakika kumi kumsifia rais Trump na kusisitiza raia wa nchi hiyo kushirikiana na rais wao ili kuimarisha nchi hiyo, na baadaye rais Trump alimsifu kwa kumwambia amezungumza jambo zuri sana.

Pia alisisitiza kuwa kuna baadhi ya watu walimshawishi asivae kofia hiyo lakini yeye hakujali kwasababu inamfanya kuwa imara na mwenye nguvu.

“wamejaribu kunitisha, marafiki zangu kuhusu kuvaa hii kofia, lakini hii kofia inanipa nguvu”

Kwa upande wa Rais Trump alipoulizwa na waandishi wa habari kama ana mpango wa kuwania tena urais alijibu kuwa” inaweza ikawa vizuri” na kanye west akasisitiza kuwa wasifikiri ya baadaye wanapaswa kujenga ya sasa kwanza.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW