Burudani

Kanye aikimbia familia akitaka kuachia Album

Baada ya kufuta akaunti zake za mitandao ya kijamii ya Instagram na twitter, Kanye West anatarajia kuachia album yake .

Album hiyo imeanza maandalizi ambayo mpaka sasa ni wiki mbili tangu rapa huyo aamue kujitenga na kuhamia sehemu za milima. Watu wameanza kuhisi huenda wawili hao, yaani Kim and Kanye wamegombana ndio maana Kanye hakuonekana wiki iliyopita katika usiku wa Met Gala na baby mama wake Kim kama ilivyo kawaida ya wawili hao.

Mara ya mwisho kwa wawili hao kuonekana kwa pamoja ilikuwa kwenye chakula cha usiku wakati wa Valentine. Kanye hajaonekana hata kwenye uzinduzi wa mavazi yake ya Yeezy. Na mpaka sasa hajawahi kufanya show yoyote tangu alipotoka hospitali mwaka jana Novemba.

Japo chanzo cha karibu cha familia hiyo kimesema kuwa Kanye ameamua kukaa mbali kidogo sio kwamba ni matatizo ya kinyumbani, wala sio tatizo la kichwa au stress, bali tu anataka kutengeneza mziki mzuri.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents