Burudani

Kanye West ahukumiwa kifungo cha nje cha miaka 2 na saa 250 kuhudumia jamii

Msanii wa muziki wa kutoka nchini Marekani Kanye West, hajakana wala kukubali mashtaka ya kumshambulia mpiga picha katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Los Angeles.

Kanye-West

Adhabu yake ni kifungo cha nje cha miaka miwili na ameshurutishwa na mahakama kupata ushauri nasaha kuhusu anavyoweza kudhibiti hasira. Pia ametakuwa kuhudumia jamii kwa masaa 250 kwa kosa hilo alilofanya Julai mwaka jana.

Mpiga picha Paparazzi ,Daniel Ramos, alimtuhumu muimbaji huyo kwa kumpiga makonde na kumpokonya kamera yake.

Muimbaji huyo mwenye umri wa miaka 36 anasisitiza kuwa hana hatia.

Mpiga picha huyo anadai kuwa bado anatumia dawa kwa ajili ya majeraha aliyoyapa kutokana na kushambuliwa na West.

“Nilikuwa nafanya kazi yangu wakati West aliponishambulia, ” alisema mpiga picha huyo, ” ikiwa ni mimi ningekuwa nimemfanyia kitendo hicho ningekuwa kizimbani.”

Ramos pia alidai kuwa alihofia kulipiza kisasi baada ya matamshi ya muimbaji huyo kupitia kwenye televisheini.

West alikamatwa mwaka 2008 kufuatia vurumai lengine na mpiga picha katika uwanja huohuo wa ndege.Kesi hiyo, ilitupiliwa mbali na mahakama baada ya West kuwalipia vifaa vilivyoharibika na pia kupata ushauri nasaha kuhusu namna ya kudhibiti hasira zake.

Source:BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents