Habari

Kanye West na Kim Kardashian wapanga kufanya harusi ya $mil.20

Kim Kardashian anadaiwa kuwa kwenye mipango ya kufanya harusi ya kifahari na Kanye West itakayogharimu dola milioni 20.

Nyota huyo wa reality TV show, ambaye amekuwa na uhusiano na Kanye kwa miezi nane sasa na hivi karibuni kurejea toka kwenye mapumziko ya Rome hadi Venice kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, anadaiwa kutaka kuvaa shela yenye gharama ya dola milioni 8 muda mfupi akipata taraka yake kutoka kwa mume wake wa zamani Kris Humphrie.

Chanzo kimoja kimeliambia jarida la OK! Kuwa Kim ameshaanza kuwasiliana na waandaji wa shughuli za harusi.

Staa huyo wa ‘Keeping Up With The Kardashians’ anadaiwa kuwa na mpango wa kumwalika mmoja kati ya Beyonce ama Celine Dion kuimba kwenye harusi yake.

“Kim’s all-time favourite singer is Celine Dion, and she has had her people reach out to her for a price; usually a private performance runs well over $6 million.Another option they’re strongly considering is Beyonce, who will be there anyway,” kilisema chanzo hicho.

“Kim’s dream dress would have real pearls and white diamonds, like the [gown] designed by Yumi Katsura, which cost $8.5 million.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents