Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Kasuku asaidi kutoa ushahidi katika kesi

Mwanamke mmoja nchini Marekani, atahukumiwa kifungo baada ya kupatikana na hatia ya kumuwa mumewe.

Mwanamke huyo aitwaye Glenna Duram kutoka jimbo la Michigan alimuua mumewe kwa kutumia risasi mnamo mwaka 2015 tukio ambalo lilishuhudiwa na kasuku.

Kasuku huyo aitwae Bud ametumika katika kutoa ushahidi baada ya kuwa ni moja ya walioshuhudia tukio hilo kabla ya marehemu kufariki kwa kukurudia manemo ya mwanaume aliyepigwa risasi aliyesema “usipige risasi”.

Bi. Duram amekutwa na hatia na jaji wa mahakama baada ya ushahidi kutolewa na ndege huyo na kupelekea mahakama kutoa maamuzi ya kumpatia hukumu mwezi Agosti mwaka huu.

Na Laila Sued

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW