Burudani

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo ampongeza msanii Monalisa baada ya kushinda tuzo hii nchini Uganda

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo ampongeza msanii Monalisa baada ya kushinda tuzo hii nchini Uganda

Leo tarehe 08/11/2018 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) Bi. Joyce Fissoo amempongeza na kumtaka Mwanatasnia wa Filamu Bi. Yvonne Cherrie Maarufu kama Monalisa kuwa Balozi mzuri wa Tasnia ya Filamu nchini mara baada ya kupata Tuzo ya heshima kutoka nchini Uganda.

Pongezi hizo amezitoa leo ofisini kwake Mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam alipokutana na Muigizaji huyo kuzungumzia masuala mbalimbali ya Maendeleo ya Tasnia ya Filamu na Michezo ya Kuigiza nchini.

Bi. Fissoo alimkumbusha Monalisa na Wadau wote wa Sekta ya Filamu na uigizaji umuhimu wa kuendelea kutoa taswira chanya katika jamii hatimaye kuwa mfano wa kuigwa kwenye jamii.

“Wewe ni mfano wa kuigwa katika jamii kutokana na kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, kuithamini na kuiheshimu kazi yako, niwakumbushe Wadau wote kujifunza yale mambo chanya kutoka kwako” Alisema Fissoo.

Kwaupande wake Monalisa alimshukuru Katibu Mtendaji Bi. Fissoo kwa kuendelea kuwapa ushrikiano akiwepo yeye mwenyewe na Bodi kuwa sehemu ya kuhimiza na kusimamia Maendeleo ya Tasnia ya Filamu na Michezo ya Kuigiza nchini. Monalisa alimuahidi kuendelea kushirikiana na Bodi hiyo katika kuendeleza na kutangaza sekta nzima ya Filamu kila apatapo fursa ndani na n je ya nchi.

“Bodi ya Filamu imekuwa ni muhimili mkubwa katika kuiongoza Tasnia ya Filamu nchini hivyo nitahakikisha naendelea kushirikiana nayo bega kwa bega ili tuweze kuipa heshima Tasnia na nchi yetu kwa ujumla kupitia kazi bora tutakazo zizalisha” Alisema Monalisa.

Monalisa amepata Tuzo ya heshima kama Mwanamke wa Mfano na mwenye Ushawishi kwa Jamii kupitia kazi zake za Uigizaji ambapo Tuzo hiyo kutoka nchini Uganda atakabidhiwa Tarehe 1 Disemba 2018 jijini Kampala.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents