Habari

Kidumu akwama nchini Canada, anyang’anywa passport yake

Msanii mzaliwa wa Burundi aishiye nchini Kenya Kidumu amekamatwa nchini Canada baada ya kuzuka ugomvi na waandaji wa ziara yake nchini humo.

Msanii huyo wa hit ya ‘haturudi nyuma’juzi alijikuta akikwama nchini Canada baada ya passport na tiketi yake ya ndege kushikiliwa.

Kidumu alikuwa amezindua albam yake mpya iitwayo ‘Kimbia’ na kuamua kwenda ziarani Marekani na Canada kuipromote zaidi albam hiyo.

Ziara hiyo ambayo imechukua miezi kadhaa ilikuwa imalizike juzi Jumamosi.

Kwa mujibu wa vyanzo, Kidumu hakuweza kurejea nchini Kenya hiyo juzi ambapo alitakiwa kuwa na show jana lakini hawezi kusafiri mpaka suala hilo litakapomalizika.

Vyanzo hivyo vimedai kuwa ugomvi huo umetokana na kuhitirafiana kuhusiana na mapato waliyoingiza na jinsi ya kugawana hali iliyopelekea maafisa wa uhamiaji nchini humo kumkamata na kuchukua nyaraka zake za kusafiria.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents