Burudani

Kilio cha wasanii nchini Kenya hatimae kimejibika!

Baada ya kukaa ndani kwa mda wa miezi zaidi ya sita ndani ya nyumba bila kupiga show wala kuhudhuria matamasha yeyeyote kwa marufuku ya kutotangamana iliyowekwa na serekali ya nchi ya Kenya, wasanii wa muziki wanakila hatua ya kutabasamu baada ya kualikwa kuhudhuria na kuwaburudisha wananchi na viongozi mbalimbali wa ngazi za juu kwenye mji wa kitalii wa Mombasa.

Tamasha hili ambalo limepangiwa kufanyika kwenye ukumbi mpya wa kifahari na wenye hadhi na maandhari yakuvutia ya kitalii maarufu kama Mama Ngina Water front, limekusudiwa kushangilia siku ya utalii duniani.

Wasanii wakubwa wa nchini Kenya kama Khaligraph Jones, King Kaka, Tanasha Donna, Masauti, Dogo Richie, Susumila na wengineo ni miongoni tu ya baadhi ya mastaa ambao wanatarajiwa kutoa burudani kwenye tamasha hilo la kwanza kuwahi kufanyika baada ya Corona.

Inasemekana kua wageni wakiwemo maafisa wa ngazi za juu serekakini pia watahudhuria kongamano hilo, ambapo inashukiwa raisi Wa Kenya Uhuru Kenyatta huenda akawa mgeni mashuhuri huku akiandamana na mwenyeji kiongozi mkuu wa jimbo la Mombasa gavana Joho maarufu kama gavana 001.

Habari zakuwepo kwa tamasha hili zimepokekewa kwa mbwembwe na matumaini ya kufunguliwa kwa uchumi wa nchini Kenya. Tayari Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta anatarajiwa kutangaza kufunguliwa kwa uwanja wa michezo wa kimataifa wa Nyayo na nyanja zingine, ili kuurudisha rasmi ratiba ya ligi tofauti za michezo na riadha Kenya.

Imeandikwa na muandishi Changez Ndzai- Kenya

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents