Burudani

Kim Kardashian avunja ukimya kuwa alimfundisha mume wake Kanye West kabla ya kwenda kuonana na Trump White House

Kim Kardashian avunja ukimya kuwa alimfundisha mume wake Kanye West kabla ya kwenda kuonana na Trump White House

Mrembo na mwanamitindo mkubwa duniani kutoka nchini Marekani Kimberly Noel Kardashian.,kwa jina la kisanii Kim Kardashian ameamua kuvunja ukimya kuhusu kuonana na Trump.

Mrembo huo amefunguka mengi sana na kuongelea suala la mume wake Kanye West kwenda kuonana na Rais wa Marekani Donald Trump na kusema yeye alihusika kwenye safari hiyo kwa asilimia zote.

Kim alisema ” Kanye West hata kama ni muimbaji na rapper mzuri sana duniani haimaanisha kuwa ndio muwasilishaji wa mpangilio mzuri wa maneno,Kiukweli hayuko vizuri kwenye mambo ya kisiasa”

Hayo aliongea Kim akiongezea Mume wake ilitokea tu kumkubali Trump na sio kwamba ana malengo ya kuwa mwanasiasa, lakini hajui chochote kuhusu mambo ya kisiasa’

Akiongea latika mkutano wa uundaji mpya wa makosa ya jinai Kim aliongeza ” Kanye ni mgumu kuelewa na uwasilishaji wake wa maneno ni mbaya nilimchagulia maneno azuri na nikamfundisha nahisi alipata shida sana, alikuwa akisema mara kwa mara yeye alikuwa ni rafiki mzuri wa Trump na bado urafiki wao unaendelea hadi sasa,nadhani ndio kilichomfanya aende kuonana nae narudia tena hayuko vizuri kwenye uwasilishaji lakini kwa anachokipigania nahisi yuko sahihi kwani ni kitu anachopenda hata kama ni tofauti na wewe unachopenda”

Kim akiongelea ugumu wa Kanye wa kujifanya anajua pia kuhusu kumuunga mkono Trump alisema:-

” kwahiyo najua hakusema ooh yeah, najua yote kuhusiana na haya na kinachoendelea kuhusiana na wageni na najua jambo hili, na najua hilo. “Kama angejua kweli, angejisikia huruma sana juu yake,Kwa hivyo yeye hajawahi kusema kuwa anaunga mkono hilo. na najua iliwachanganya wengi sana kwa sababu wakati unapoona mtu amevaa kofia nyekundu [MAGA] utahisi anaunga mkono Lakini yeye anapigana tu kwa mawazo huru. Na kwa uhuru wa kupenda mtu, hata kama sio uamuzi wa kujitangaza.”

Kwahiyo hakuhitaji mtu wa kutafsiri na mimi baada ya kujua hilo nilikuwa karibu yake muda wote kwa kujua ni kitu gani anatakiwa azungumze kwani namjua sana tangu nyumbani”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents