Habari

King Kiki na ‘The Coming of Age’


Msanii mkongwe katika tasnia ya muziki wa Dansi na Rhumba Kikumba Mwanza Mpango almaarufu kama King Kiki yupo njiani kutoka na albamu ya marudio yenye nyimbo zake zilizowahi kutamba zamani.
Albamu hiyo ambayo itakuwa na jumla ya nyimbo kumi itakuwa ni marudio ya nyimbo zake kumi bora kati ya alizowahi kuziimba katika kipindi cha miaka 5o ya kuwamo katika gemu la muziki.

Akizungumza na bongo5.com nyumbani kwake leo mchana mzee King Kiki alisema tayari ameanza maandalizi ya kurekodi nyumbo hizo ambazo zitarekodiwa katika studio za Aegies studio chini ya prodyuza Nice P na kwamba alishafanya mazoezi ya nyimbo hizo.

Aidha katika maelezo yake mzee king Kiki alisema project hiyo itahusisha staili tatu tofauti za muziki ambapo ya albamu ya kwanza itakuwa na nyimbo kama “mtoto wa mjini, sababu ya nini’, na ’Sango ya bana” na Albamu ya pili itakuwa ni staili ya Jazz tu na albamu ya tatu itakuwa ni nyimbo za kolabo na wasanii mbali mbali wa Bongo flava pamoja na wengine wa ki Afrika.

Mzee King kiki alisema project hiyo inatarajiwa kuitwa “The Coming Of Age, ama Ujuzi Hauzeeki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents