Habari

Kiongozi wa Islamic State (IS) ambaye anadaiwa kuwa na uzito wa kilo 250 akamatwa nchini Iraq

Kiongozi wa Islamic State (IS), Abu Abdul Barihuyo amekamatwa leo Jumatatu Januari 20 na kubebwa na lori kutokana na kuwa na uzito mkubwa baada ya kushindwa kuingia katika gari ya kawaida na kupakiwa kwenye roli kwa kwa madai kiongozi huyo ana kilo 250.

Serikali ya Iraq kupitia taarifa yake imedhibitisha kukamatwa kwa kiongozi huyo ambako maofisa wa usalama walisema kuwa kiongozi huyo wa ugaidi alikamatwa na kikosi maalum cha silaha cha kijeshi (SWAT) Kusini Mashariki mwa mji wa Mosul nchini Iraq.

Baada ya kukamatwa kwa kiongozi huyo maarufu kwa jina la Shifa al-Nima ambaye alikuwa mstari wa mbele katika kundi hilo alisafirishwa kwenda gerezani kwa kutumia lori hilo.

Picha za Bari ambaye polisi wa Iraq wanamtambua kama mwandamizi wa kundi la IS zilizoonyesha akiwa amepakizwa kwenye lori akiwa katika ulinzi mkali wa polisi waliokuwa na silaha.

Bari ni mufti wa kundi la IS na mtaalamu wa sheria za dini ambaye aliidhinisha fwata iliyosababisha vifo vya wafuasi ambao walikataa kujiunga na kundi hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents