Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Kisutu: Mama Wema aonywa na Hakimu Mahakamani

Mama Mzazi wa  msanii wa filamu za Bongo, Wema Sepetu  Miriam Sepetu , ameonywa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba baada ya mtoto wake huyo kutohudhuria mahakamani kwaajili ya kuhudhuria katika kesi  ya matumizi ya madawa ya kulevya inayomkabili.

Wakili wa Serikali Agustino Michael ambaye ni Wakili wa serikali aliitaja kesi hiyo mbele ya hakimu Simba kuwa ndiyo iliyokuwa ikitakiwa kuendelea.

Mama wa mrembo huyo alinyoosha kidole na Hakimu alimkaribisha mama huyo kusema, mama huyo ameiambia mahakama kuwa mwanae ameshindwa kufika mahakamani hapo kwa kuwa amefiwa na shangazi yake hivyo ameenda kushughulikia shughuli za mazishi ndiyo maana hajafika na mimi nimekuja kumuwakilisha.

Baada ya mama huyo kutoa hudhuru huo, Hakimu  alimuuliza kama Wema amepatwa na msiba uliomfanya ashindwe kufika mahakamani imekuwaje yeye mama huyo apate muda huo yeye ashindwe?

Hata hivyo Hakimu alimueleza mama huyo na kumuambia asichukulie masihara suala la mstakiwa kuripoti Mahakamani. Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Disemba 14 mwaka huu.

 

 

 

Leave a comment

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW