Habari

Kituo cha polisi chashambuliwa mjini Mombasa, Kenya na polisi kadhaa kuuawa

Takriban polisi wanne mjini Mombasa, Kenya, waliokuwa wamesambazwa kuhakikisha amani kwenye uchaguzi wa urais unaofanyika leo wamevamiwa na kuuawa na kundi la watu saa chache kabla ya vituo vya kupigia kura kufunguliwa.

kenyavote1.jpg.size.xxlarge.letterbox

Kwa mujibu wa BBC washambuliaji waliokivamia kituo cha polisi mjini Mombasa wanashukiwa kuwa wafuasi wa kundi la Pwani la Mombasa Republican Army (MRC) ambao wamekuwa wakipigania uhuru wa jimbo la Pwani.

Hata hivyo shambulizi hilo huenda halihusiani na masuala ya uchaguzi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents