Michezo

Kocha wa Arsenal Unai Emery atema cheche ” Mabadiliko yanahitaji muda, hatuna uwezo wa kununua mchezaji kwa sasa labda tuchukue kwa mkopo”

Kocha mkuu wa klabu ya Arsenal Mhispanyola Unai Emery amefunguka na kuweka wazi hisia zake na maoni yake kutokana na kile kinachoendelea mitandaoni hasa kuhusu yeye na timu yake.

Kauli yake hii inakuja baada ya mashabiki wa Arsenal kuazna kulaumu kuhusu kiwango cha timu hiyo kwani imeanza kudorora baada ya mwanzo kufanya vizuri katika baadhi ya michezo.

Wakati klabu inabadilisha meneja, ni kwa sababu wanataka kitu kipya, “anasema.” Changamoto ni kutambua kitu kizuri ni kipi – ni kitu ambacho unayopaswa kukitunza – lakini pia mambo unayohitaji kubadili na kuboresha. Hapa, ni wazi, kulikuwa na mambo mengi ya kubadili na kuboresha. “

Baada ya kufunguka kuhusu hilo pia aliongelea kuhusu kununa wachezaji wapya na alisema ” “Hatuweza kusajili mchezaji mwingine kwa kutoa hela mfukoni labda tuchukue mchezaji kwa mkopo, hicho nahisi haukutarajia kusikia kutoka kwenye klabu iliyoko nyuma kwa alama 6 kutoka kwenye timu iliyoko top four, ikiwa na hatari ya kutokushiriki michuano ya kimataifa kwa mara ya tatu mfululizo baada ya miaka 19 ya kucheza katika michuano mikubwa ya kimataifa”.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents