Michezo

Koscielny afunguka baada ya kustaafu timu ya taifa ” Nilitamani Ufaransa wapoteze kombe la dunia”

Nilikuwa mbinafsi sana

Beki wa klabu ya Arsenal na aliyewahi kuwa beki wa timu ya taifa ya Ufaransa Laurent Koscielny amefunguka mwanzo mwisho baada ya kustaafu kuitumikia timu yake ya taifa ya Ufaransa.

Koscielny ameongea hayo wakati anazungumza na kituo cha habari cha kifaransa cha Canal+ mara tu baada ya kutangaza kustaafu soka lake la kimataifa.

Amesema “Majeraha yangu yalikuwa vigumu kukubali , Na majibu yakawa magumu zaidi baada ya matokeo kushinda Kombe la Dunia. “Nilikuwa mbinafsi sana na mwenye wivu, nilikuwa najiuliza na kujiuliza na kutamani hata mimi ningekuwa sehemu ya waliofanikiwa kushinda Kombe. na hilo ndo lilikuwa miongoni mwa mafanikio yangu katika maisha yangu yote ni vigumu na hakuna mtu anayeweza kujiweka katika viatu vyangu.”

“Nilifurahi sana kwa ushindi wao, lakini pia iliniumiza sana kwa upande mwingine,  Huwezi kujihis na kujisikia kama miongoni mwa mabingwa wa kombe la dunia kama ilivyokuwa kwa zaidi ya Wafaransa milioni 60,Nilikuwa na  hisia za ajabu sana wakati wa mashindano kuna upande nilitaka wafuzu , lakini wakati huo huo nilitaka wapoteza. Hiyo ilikuwa hisia yangu wakati huo wote wa mashindano”

Aliongeza ” Haya yalikuwa majereha makubwa kwangu kwa mara ya kwanza maana nilijiweka vizuri kifikra kiakili nguvu kila kitu nilijifunza vingi sana katika mpira lakini sasa natengana na familia yangu”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents