Michezo
Kuelekea mchezo wa #ElClásico, Lionel Messi na Dembele wazua hofu Barcelona
Washambuliaji wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi na Ousmane Dembele huenda kesho wakakosa mchezo wa kwanza wa Copa Del Rey dhidi ya Real Madrid.
Dembele jana alianza mazoezi ya kwake peke yake baada ya kukaa nje kwa wiki mbili akiuguza majeraha huku Messi akikosa kabisa kuhudhuria mazoezi baada ya kuumia wiki iliyopita kwenye mchezo dhidi ya Valencia.
Mchezo huo wa El-Clasico utapigwa kesho usiku kunako dimba la Camp Nou.