Tupo Nawe

Kufuru: Mayweather atuonyesha sehemu za utajiri wake na vitu vya thamani anavyomiliki (+ Video)

Bondia wa Marekani, Floyd Mayweather alimaarufu kama ‘Money Man’ ameibuka nakuanza kuonyesha baadhi ya sehemu zake za utajiri. Mbali na bondia huyo kuonyesha sehemu hizo pia ameonyesha baadhi ya vitu anavyomiliki vya thamani kama Gari, nyumba, saa za thamni kubwa, ndege yake binafsi na vitu kibao.

Mayweather amekuwa kwenye baadhi ya migogoro na mastaa wakubwa akiwemo mpiganaji wa MMA kutoka nchini Ireland pamoja na Rapper kutoka nchini humo 50 Cent, ambao walikuwa wakimtupia maneno makali baada ya kutangaza kupambana na bondi mwenye umri mdogo zaidi kutoka nchini Japan, huyu si mwingine bali ni Tenshin Nasukawa.

Katika pambano hilo Mayweather aliwajibu yeye anachoangalia ni pesa na sio kingine, na hilo lilikuwa ni jibu kwa hao mastaa wawili ambao ni 50 Cent na Mc Gregor.

Sasa swali linakuja kwamba Mayweather kutuonyesha baadhi ya sehemu ya utajiri wake litakuwa ni dongo kwa hawa watu wawili ? Ingawa tumejaribu kufanya uchunguzi kuona kama jamaa watamjibu lakini bado.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW