Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Kuibuka kwa wizi wa nywele za Wanawake usiku

Zaidi ya wanawake 50 katia majimbo ya Kaskazini mwa India ya Haryana na Rajasthan wamesema kuwa wamekatwa nywele zao wakati wakiwa hawana fahamu kitendo cha kinachowaacha na mshutuko mkubwa.

Sunita Devi

Sunita Devi mwanamke mwenye umri wa miaka 53 kutoka Haryana alieleza kuwa kulikuwa na mwanga mkali uliomsababisha kupoteze fahamu na baada ya saa moja kupita aligundua kuwa nywele zake zimekatwa.

Pia mwanamke mwingine aitwae Asha Devi alipoteza nywele zake katika tukio kama hilo, hata hivyo inaelezwa kuwa wanaofanya matuki hayo ni wanawake.

Shuda wa tukio hilo Pal alisema alikuwa nyumbani wakati Asha Devi akitoka nje kufanya kazi zake. “Nilienda nje kujua ni kwa nini hakurudi baada ya zaidi ya dakika 30, tulimkuta amapoteza fahamu bafuni na nyele zake zilikuwa zimekatwa na kutupwa sakafuni,” alisema.

Taarifa za kunyolewa nywele wanawake zilianza kuibuka mapema July mwaka huu kutoka jimbo la Rajasthan, lakini pia matukio kama hayo yameripotiwa kutoka Haryan na mji mkuu Delhi.

By Peter Akaro

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW