Aisee DSTV!

Kuna kitu cha kujifunza katika video hizi 2 mpya za Burundi zinazochezwa Trace TV

Tasnia ya muziki nchini Burundi ina jambo la kusherehekea mwezi huu baada ya video mbili za wasanii wa huko kupitishwa na kuanza kuchezwa kwenye kituo maarufu cha muziki cha Trace Urban TV. Hiyo ni mara ya kwanza kwa wasanii wa Burundi.

10501765_298713010300375_4936241845904466924_n

Nyimbo hizo ni pamoja na ‘Jigi Jigiwe’ ya Happy Famba na Katoto Rmx ya Dj Pro aliyewashirikisha Sat B & Mkombozi. Video zote zimeongozwa Kent P. Kwa mujibu wa mtangazaji wa Rema FM na Rema TV ya Bujumbura, Ismail Niyonkuru, kuchezwa kwa video hizo kumepokelewa kwa shangwe kubwa na wananchi wa Burundi wakichukulia hatua hiyo kuwa muhimu katika muziki wao ambao hufanywa kwa Kiswahili zaidi.

10563181_298713063633703_7713475847731002296_n

Ikumbukwe kuwa kupata nafasi ya kuchezewa video yako Trace TV si jambo rahisi. Kwa Tanzania ni Diamond, AY na wengine wachache pekee waliofanikiwa kuchezewa video zao huko. Tujiulize imewezekana vipi kwa video iliyoongozwa na director asiye na jina kubwa Afrika kuwashawishi Trace TV? Tunawapa pongezi wasanii hao.

Muhimu: Habari tumeiandika kwakuwa tuna wasomaji wengi nchini Burundi na tungependa kuungana nao katika furaha yao

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW