Burudani

Kuna kitu kimeturudisha nyuma Yamoto Band – Aslay

Mmoja kati ya wasanii wanaounda Kundi la Yamoto Band, Aslay, ambaye hivi sasa ameanza kufanya kazi peke yake nje ya kundi hilo, amefunguka kwa kudai kuwa kuna vitu vimewakwamisha na kushindwa kwenda mbele kama kundi.

Yamoto Band

Muimbaji huyo amedai kipindi cha nyuma walikuwa wanapata show nyingi sana jambo ambalo lilipelekea kuwa na uwezo wa kufanya video kubwa hata nje ya nchi lakini baadaye mambo yalibadilika na kupelekea kufanya video zao hapa hapa bongo.

“Mimi nafikiri kwamba mipango yetu tu wenyewe, kipindi kile tunatoa ile video ‘ Madoido’ kulikuwa na show nyingi zinaongozana ambazo zilituzuia kwenda kutengeneza video nyingine lakini si unajua tulikuwa tunajenga pia kwa hiyo kifupi ni kama tulijisahau na kuteleza kusema ukweli,” alisema Aslay.

Aliongeza, “Tukarudi tena tukafanya ‘Suu’ ambayo tuliifanya Zanzibar na tukawa na pesa kabisa ambayo ingetuwezesha kutengeneza video nyingine Afrika Kusini lakini hapo katikati tulifanya vitu fulani mchanganyiko ambavyo siwezi kuvisema vikaturudisha tena nyuma” alisema Aslay

Mbali na Aslay msanii mwingine kutoka kundi hilo Beka Flavour naye ametoka na wimbo wa peke yake akiwa chini ya menejimenti nyingine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents