Habari

Kupima UKIMWI ni lazima nchini Zambia

Rais wa Zambia, Edga Lungu ameamuru kuwa kila raia nchini humo ni lazima apimwe ugonjwa wa ukimwi ili kuliweka taifa katika uwazi kuhusu takwimu za waathirika .

Tokeo la picha la Edgar Lungu
Rais wa Zambia, Edgar Lungu

Zambia inatajwa kuwa ni kati ya nchi zenye viwango vya juu zaidi vya maambukizi ya UKIMWI kusini mwa bara la Afrika kwa asilimia 11.6, huku watu walio na umri wa kati ya miaka 15 na 49, wakiwa wanaishi na virusi vinavyosababisha UKIMWI.

Rais Lungu amesema kuwa kupimwa na kupewa ushauri na matibabu sio kitu cha kujitolea, katika jitihada za kukabiliana na ugonjwa wa ukimwi nchimi humo.

Lungu alitoa tangazo hilo wakati wa uzinduzi na baraza la ukimwi kwenye mjini Lusaka,Bwana Lungu alisema kuwa suala hilo limezungumziwa na baraza la mawaziri lengo haswa likiwa ni kukomesha gonjwa hilo hatari.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents