Habari

Kutana na rapper mwenye umri mkubwa zaidi duniani

Kama ulidhani Bi. Cheka ndo msanii mwenye umri mkubwa zaidi anayeimba nyimbo za vijana Afrika Mashariki basi you are wrong! Here comes World’s Oldest Rapper – Lucy Ntambi from Uganda.
Lucy Ntambi aka Ragga Queen ameibuka na kuwa rapper mwanamke mwenye umri mkubwa zaidi duniani. Pamoja na umri wake she still got the killa swag!
Akiwa na umri wa miaka 86, hivi karibuni Lucy Ntambi ameachia ngoma iitwayo ‘Ebyenyanja‘ unaomaanisha ‘samaki’.
Wimbo huo unalaani uvuvi haramu wa samaki katika ziwa Victoria na mtiririko wa mawazo kwenye ngoma hiyo ni wa maana. Bibi yuko fit.
Anakiita kitendo hicho kama tamaa na pia kuwashambulia waganda waliouza rasilimali za nchi hiyo kwakuwa wanapenda pesa zaidi kuliko ustawi wa nchi yao.
Kingine Bibi Ntambi anazungumzia jinsi waganda wanavyokula mabaki ya samaki ‘mapanki’ na minofu kusafirishwa nchi za nje.
Katika video ya wimbo huu, Bibi huyo anapewa shavu na wajukuu zake wawili huku wakionekana wakicheza kwenye mdundo huo wakati ambapo bibi yao akiendelea kuchana mistari like a teenager!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents