Kama sio DStv potezea
TECNO Spark 2

Habari

Kwanini matukio ya Kibiti hayaleti mshtuko mkubwa? – Mkuu wa Majeshi

By  | 

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo amehoji kuwa matukio ya yaliyokuwa yakiendelea Kibiti hayaleti mshtuko mkubwa sana wakati watu waliothirika ni wengi zaidi kuliko matukio ya sasa?.

Jenerali Mabeyo ameyazungumza hayo na kuhoji kwenye mkutano wake na waandishi wa habari na kusema kuwa kwa sasa wananchi hawatakiwi kuwa na majibu ya haraka wanataka kujiridhisha kuwa silaha hizo zinatoka wapi na ni watu aina gani.

“Kama yale matukio ya Kibiti, kwanini matukio ya Kibiti hayaleti mshtuko mkubwa sana sasa wakati watu waliothirika ni wengi zaidi kuliko matukio ya sasa?,” alihoji Mobeyo.

“Mimi sitaki kuingia huko, lakini nasema vyombo vya ulinzi na usalama wakati wote vinakabiliana na matukio kadili yanavyojitokeza, na ninaamini hali itakuwa shwari na sasa vinashughulika, hoja ya msingi tunataka kujiridhisha silaha hizi zinatoka wapi? Hawa watu ni wa aina gani sasa vyombo mviachie vifanye kazi yake msitoa majibu haraka.”

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments

Bongo5

FREE
VIEW