Habari

Lady Gaga kujenga nyumba inayoelea baharini nchini Ugiriki


Katika kuonesha kuwa si tu katika mavazi yake anayovaa hupenda kuwa tofauti, mwanamuziki wa pop nchini Marekani Lady Gaga anajenga nyumba ya kifahari nchini Ugiriki itakayokuwa ikionekana ikielea juu ya bahari.
Nyumba hiyo ambayo inamgharimu kiasi cha paundi milioni 10, inajengwa mjini Crete ambako mwanamuziki huyo wa ‘Born This Way’ alinunua kiwanja mwaka jana.
Vyanzo vimeliambia gazeti la Daily Star kuwa nyumba hiyo ikikamilika itakuwa ya kipekee.
Mwimbaji huyo mwenye miaka 26, ana mpango pia wa kuwa na ikulu yake na kanisa lake mwenyewe kwenye ardhi ya Ulaya.
Chanzo hicho kimeeleza kuwa nyumba hiyo inajengwa majini na kama kuna mtu atataka kuiona ni lazima apande boti.
“Licha ya ikulu na kanisa, mradi huo utakuwa na kiwanja cha tennis na mabwawa mawili ya kuogelea.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents