Burudani

Lamar: Producer na wasanii wa Bongo wabadilike, ‘find your own sound’

Producer Lamar ametoa ushauri kwa watayarishaji wenzake wa muziki nchini kubadilika na kutafuta utambulisho wao wenyewe kuliko kugeza kila midundo mizuri wanayohisi inapendwa.

230002_10150183701685740_5642298_n

“Artists na producers need to change, find you own sound,” alisema Lamar kwenye mjadala na Bongo5. “Sound wewe kama wewe, usijaribu kuwa copycat kwamba labda katengeneza beat kali Marco Chali na wewe unataka isound hivyo hivyo sababu ipo kwenye peak, no..tengeneza kitu chako, buni kitu chako. Na wasanii sio mnataka kuigana kwamba Diamond akitoa hit ‘ahh nitengenezee beat kama ya Diamond, vitu haviendi hivyo.

Tutengenezee genres tofauti, kuwe kuna R&B, kuna Pop, Soul, Jazz kila mtu anafanya muziki aina yake wasistick kwenye Bongo Flava tu. Kwasababu kama unataka kwenda international inabidi ucheze muziki wa kimataifa. Uchezaji wa chords uwe tofauti. Kuwe na kuna elements za Bongo Flava unachanganya na international tunaweza kufanya vizuri.”

[soundcloud url=”https://api.soundcloud.com/tracks/128296754″ params=”color=ff6600&auto_play=false&show_artwork=true” width=”100%” height=”166″ iframe=”true” /]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents