Shinda na SIM Account

Lina Iris amshtaki Kendrick Lamar kwa kuiba mchoro wake na kutumia katika video ya All The Stars

Mwanadada Lina Iris Viktor ambaye ni mzaliwa wa Liberia lakini amekulia jijini London nchini Uingereza. Lina ni mchoraji mzuri sana ambaye anaishi na kufanya kazi kati ya New York na London.

Lina ameanzisha kesi dhidi ya Black Panther kwa kutumia mchoro wakebila ridhaa katika nyimbo ya Kendrick Lamar na SZA“All The Stars”kutokana na taarifa walizo zitoa The New York Times.

Ripoti hizo zinasema kuwa wawakilishi wa Black Panther waliwasiliana kwa mara kadhaa na Lina Viktor na kumuambia wanaomba kutumia kazi zake katika video ya All The Stars lakini Lina Viktor alikataa ofa hiyo ya Marvels.

Christopher Robinson, mwanasheria wa Lina Viktor, aliwasiliana na Anthony Tiffith wa Top Dawg Entertainment Jumamosi Februari 10 mwaka huu kuhusu ukiukaji wa hakimilik ya bidhaa ya Lina Viktor .


Lina aliiambia The New York Times, “It’s an ethical issue, because what the whole film purports is that it’s about black empowerment, African excellence — that’s the whole concept of the story. And at the same time they’re stealing from African artists.”

Kendrick aliwashukuru kila msanii aliyehusika na albamu Black Panther katika ujumbe alioutuma kwenye mtandao wa Twitter siku ya Jumapili Februari 11.

Na Raheem Rajuu

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW