Burudani

Linah kudondosha songi jipya siku ya Eid Mosi


Mwanamuziki wa kundi la THT Linah Sanga anatarajia kuzindua wimbo wake mpya siku ya Eid Mosi kwenye viwanja vya Dar Live jijini Dar es Salaam.
Linah ambaye miezi ya hivi karibuni alikuwa kwenye ziara ndefu ya nchini Marekani, amesema wimbo huo unaitwa ‘Ushafahamu’.
Akiongea na Jambo Tanzania ya TBC1 jumamosi August 18, 2012, Linah amesema wimbo wake huo ni wa mapenzi na amemuiambia mpenzi wake.
Aliongeza kuwa hiyo itakuwa mara ya kwanza kutumbuiza Dar Live na kwamba ziara yake ya Marekani imemuongezea uzoefu zaidi katika kutumbuiza jukwaani.
Linah alisema kuwa kwa sasa sio Linah yule wa zamani kutokana na kuendelea kukua zaidi kisanaa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents