Michezo

Lionel Messi, Cristiano Ronaldo vita bado ngumu barani Ulaya (+video)

Washambuliaji wa klabu ya Barcelona na Juventus, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo bado ushindani wao barani Ulaya unaendelea kuwa mgumu baada ya wawili hao usiku wa jana kila mmoja kutupia goli mbili.

Ronaldo na Messi

Messi usiku wa jana aliikoa Barcelona kwa kufunga goli 2 dhidi ya Valencia, mchezo ambao ulimalizika kwa goli 2-2 katika dimba la Camp Nou.

Wakati Messi akitupia goli mbili, mpinzani wake Ronaldo naye pia alitupia goli 2 kati ya tatu zilizofungwa na Juventus dhidi ya Parma.

Wachezaji hao wawili kwa siku ya jana walifanikiwa kuziokoa timu zao kutoka kwenye kipigo.

Ndani ya msimu huu wa 2018/19, Messi tayari ametupia goli 29 kwenye michezo yote aliyoitumikia Barcelona, huku Ronaldo akitupia goli 19 ndani ya Juventus. Tazama magoli yao ya jana hapa chini

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents