Habari

Lissu kupekuliwa nyumbani kwake

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema polisi wamemchukua mwanasheria mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu na kwenda naye nyumbani kwake kwa ajili ya kumpekua.

Msafara wa magari ya maofisa wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam umeongozana na Lissu ambaye ni mbunge wa Singida Mashariki na mawakili wake.

“Wamemchukua hapo kituoni na kuelekea naye hadi nyumbani, lengo ni kumkagua.Mawakili wanaomsaidia Lissu wameshaondoka muda huu ili kujua ni kitu gani atapekuliwa,” amesema Mrema.

Kaimu Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum Lucas Mkondya alipotakiwa kuzungumzia taarifa hizo alikata simu baada ya kuulizwa kuhusu upekuzi huo.

Jana Agosti 22,Lissu alinyimwa dhamana baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kumkashifu Rais John Magufuli na uchochezi.

Na Emmy Mwaipopo

Chanzo: Mwananchi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents